Star Tv

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali itawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi wa idara ya uvuvi na maafisa uvuvi kwenye halmashauri zote nchini watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu katika kutokomeza uvuvi haramu.

Add a comment

Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amewaagiza wakurugenzi na watendaji wa Shirika la Madini La Taifa [STAMICO] kutoa maelezo ya kwanini wasichukuliwe hatua kwa kuisababishia madeni Serikali ya shilingi Bilioni 54.

Add a comment

Wadau wa Kahawa mkoani Kilimanjaro wamepongeza hatua ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuvunja mfuko wa maendeleo ya zao la Kahawa (CDTF) wakieleza kuwa mfuko huo ulikuwa ni mzigo kwa wakulima kutokana na tozo mbalimbali.

Add a comment

Pamoja na Serikali kutoa bei elekezi ya Mbolea bado baadhi ya Wafanyabiashara wa Pembejeo wanauza bei ya juu ambapo mbolea ya Kupandia Shilingi 57,300 lakini wanauziwa 80,000 huku ya kukuzia ikiuzwa 60,000 badala ya 47,000 kama bei elekezi inavyoelekeza.

Add a comment

January 15, 2018 Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ametoa taarifa inayoelezea mambo aliyoyajadili wakati alipokwenda IKULU kukutana na Rais Magufuli January 9 2018.

Add a comment

Waziri mkuu wa Kassim Majariwa,amemwagiza mkuu wa mkoa wa Mara,Adamu Malima,kumchukulia hatua mhandisi wa Rorya Oberto SASAI kwa kushindwa kusimamia mradi wa maji wa kijiji cha Kinesi uliotolewa kiasi cha sh million 700 huku mkandarasi akishindwa kuukamilisha kwa wakati.

Add a comment

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ametaka ukusanyaji wa mapato katika sekta ya madini ufanyike kwa uwazi bila kificho na kuagiza kuwa kuanzia sasa kazi za kukusanya Maduhuli zinazofanywa na Ofisi ya Madini hazitafanywa na ofisi hiyo pekee bali watashirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama katika eneo husika.

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri wenye dhamana kushugulikia agizo hili mara moja.

Add a comment

Serikali imewatoa wasiwasi wakulima wa Pamba mkoani Morogoro juu ya upatikanaji wa soko pamoja na pembejeo ambapo mnunuzi atakayenunua Pamba yote itakayozalishwa amepatikana.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.