Star Tv

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nchi saba zilizochaguliwa za Kiafrika kuwa sehemu ya mkutano wa pili wa kilele wa masuala ya kiuchumi na kibinadamu uliojulikana kwa jina la Urusi na Afrika ambao ulianza Julai 27-28, 2023 huko St Petersburg.

Baada ya mkutano huo, waandishi wa habari wa Afrika walipata fursa ya kutembelea kituo cha taarifa za nishati ya nyuklia na madini urani cha Rosatom huko St Petersburg. Denis Ezurov ni Mkurugenzi mtendaji makampuni ya pamoja-Dalur. Aliwatembeza waandishi katika machimbo ya Urani ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha eneo la bwawa kubwa ambalo mchanganyiko wa Urani hupitia katika bwawa hilo kabla ya kuipita katika sehemu ya uchakataji na kuengenisha urani na vimininika vingine anasema;

‘’ Mikusanyiko yote ya madini inakusanywa kwenye bwawa hili, baada ya hapo inasukumwa hadi kwenye jengo hili ambapo mchakato unafanywa na kimsingi kuchukua Urani kutoka kwenye suluhisho. Kwa hivyo ni mzunguko ambao mikusanyiko yote ya madini inasukumwa ndani na nje bila kupoteza madini.’

Wanahabari hao baadaye waligawanywa katika vikundi viwili na wengine wakitembelea Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Leningrad huko St Petersburg wakati kundi lingine lilitembelea machimbo ya urani yaliyopo katika kijiji cha Uksyanskoe katika mkoa wa Kurgan, katika jiji la Moscow na kuona jinsi madini ya urani yanavyochakatwa kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

“Tuna maeneo matatu makuu matatu na hii ndio sehemu kuu ya machimbo ambayo tunapata karibu 75% ya madini ya urani na tumeanza kujipatia madini ya urani tangu mwaka 1997. Na eneo la tatu la machimbo linahusiana na shughuli za utafiti na majaribio. Mnamo mwaka 2012 hadi 2013 tuliboresha maeneo haya ya machimbo ili kuongeza na kuboresha uzalishaji na kuwa wenye tija Zaidi.”

Uchakataji wa madini ya urani unapita katika Vyungu vya kuchakata madini na kisha huyatengansha madini tofauti yanayopatikana ili kuyatenga na madini ya urani na kuwa peke yake. Akibainisha Mhandisi Mwandamizi, ndugu Kamol Kadyrov anasema Mhandisi Mwandamizi

“Katika sehemu ya uchakataji kuna sehemu tofauti ambapo sehemu hizi kuna moja wapo inachakata madini upya kabla ya kwenda katika sehemu nyingine. Na hii ni Baada ya madini kuwa yametulia kutoka katika uchakataji wa awali. na huu ni mkusanyiko wa madini tunayopata kutoka ardhini kabla hatujachuja kila madini yawe peke yake.

"Na hiki ni kimiminika kilichojaa urani ambayo tunayapata hapa katika uchakataji.” “Mchakato huu huenda kwanye sehemu nyingine ambayourani hugeuzwa kutoka kimiminika na kuwa katika umbo gumu na imaraSuala la machimbo ya madini ya urani Pamoja na nishati ya Nyuklia kupewa kipaumbele kwa nchi za Africa lilikuwa ni moja ya ajenda kuu iliyojadiliwa katika mkutano wa Urusi na Afrika na baadhi ya viongozi Waliohudhuria walijadili mtazamo wa maendeleo ya nishati ya Nyuklia katika eneo la Afrika na njia zinazowezekana za ushirikiano katika eneo hili.

Waziri wa Madini Tanzania ndugu Dotto Biteko ambaye ni mmoja wa waliohudhuria na kushiriki katika baadhi ya mijadala iliyohusiana na suala la nishati na madini alizungumza haya;

“Sisi kama nchi tuko tayari kumkaribisha mtu yeyote mwenye teknolojia yoyote, Hata mwenzangu amesema tunahitaji kufanya jitihada kuunganisha nguvu na kuweza kuja kwa pamoja na kuweka mikakati ya kufanya juhudi za pamoja kutengeneza mtambo wa nishati ya Nyuklia au kuzalisha aina yoyote ya nishati ya Nyuklia. Ninaamini Pia kutokana na rasilimali tulizonazo tunatakiwa kuweka nguvu zaidi ili tuje na ugunduzi mzuri utakaotusaidia katika kuendeleza nishati.’

Antonio Ondo ni Waziri wa Madini kutoka Equatorial Guinea yeye alibainisha haya;

“Kwangu mimi kilicho muhimu kuhusu mabadiliko ya nishati ni kwamba chochote tunachofanya, tunafanya hivyo kwa sababu tunataka kuboresha maisha ya watu hatuwezi kufanya chochote ambacho haimaanishi kuboresha maisha ya watu, kwa sababu tukifanya hivyo kwa nini tuko hapa.Kwa hivyo, hatua zozote tunazochukua, inapaswa kuzingatia ukweli ambao watu wanahitaji ufikiaji wa Nishati na ufikiaji wa aina ya nishati ambayo ni nafuu na ambayo inaweza kupatikana kwao bila kuathiri uhuru wao.”

Lazarus Amukeshe Mwandishi kutoka Namibia alikuwa na haya ya kusema; "Kwa hivyo  Rosatom inapanga uchimbaji madini nchini Namibia kwa kutumia teknolojia hii pia. Kwa kweli ziara hii imekuwa na manufaa kwetu kutupatia ufahamu wa kimsingi juu ya nini kinachofanywa.”

Waandishi hao wa habari kutoka Afrika walitoka Ghana, Nigeria,Kenya, Namibia, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia ambao walishiriki katika kongamano la maendeleo ya kiuchumi na masuala ya kibinaadamu kati ya Urusi na Afrika.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.