Matokeo ya utafiti uliofanywa na Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA kwa mikoa ya Arusha, Morogoro na Mwanza yanaonesha miundombinu katika sehemu ya kutolea huduma za kijamii siyo rafiki kwa walemavu hao wa kusikia ikiwemo kukosa tafsiri ya lugha ya alama wakati wakihitaji huduma.
Ingawa maisha yanasonga lakini vipo vikwazo vyenye kuwakumba wakati wakihitaji huduma kadhaa, Upo utafiti unaweka wazi vikwazo hivyo vinavyoficha haki zao Utafiti unasema Ni mara chache kukuta mkarimani katika huduma za kijamii kama hospitali na sehemu nyingine.
Hili linatia shaka juu ya mustakabali wa Viziwi nchini.
Licha ya kuwepo kwa Sera na Sheria ya Walemavu namba 9 ya mwaka 2004, utekelezaji wake unatajwa sio wa kiwango cha kuridhisha. Katika mafunzo haya wajumbe watapata fursa ya kujadili utafiti huo unaoonesha bayana yenye kuwakabili viziwi.
Picha na mtandao.