Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amewaagiza wakurugenzi na watendaji wa Shirika la Madini La Taifa [STAMICO] kutoa maelezo ya kwanini wasichukuliwe hatua kwa kuisababishia madeni Serikali ya shilingi Bilioni 54.
Ni siku chache zimepita tangu Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuishikan nafasi hiyo, na hii ni Ziara yake ya kwanza.
Dotto anawalalamikia Watendaji kwa kushindwa kuwa wabunifu na badala yake wamebweteka na kuisababishia hara hizo Serikali.
Naibu Waziri Biteko akashindwa kujiuzia kwa kusema mtu pekee ambaye anaonekana anafanya kazi vizru kwenye Shirika hilo ni Mlinzi pekee ambaye anafungua geti na magari kuingia na kutoka.
Lakini utetezi wa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo ukoje? Alex Rutagwelela anamueleza Naibu Waziri changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa mitaji snjari na kushindwa kufanya upembuzi yakinifu katika miradi yake.
Naibu Waziri Biteko amewaeleza Wakurugenzi hao kuwa Serikali ya wamu ya tano inategemea zaidi pato lake kupitia sekta ya madini lakini kwa mwenendo huo wa Stamico unamtia shaka Naibu Waziri kutokana na kila mradi unaotajwa na Shirika hilo unahasara.
Picha na mtandao.