Star Tv

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini. Sherehe ya kuwakaribisha viongozi hao itafanyika Jumanne asubuhi katika Majengo ya Muungano huko Pretoria kabla ya Mkutano wa 15 wa BRICS utakaofanyika tarehe 22 - 24 Agosti 2023.

Ziara ya Kiserikali itafanyika katika muktadha wa kuadhimisha miaka 25 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya wawili hao. Huku historia ya uhusiano ilianza katika mkutano wa Bandung wa 1955. Mahusiano kati ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Watu wa China yanatawaliwa na Ushirikiano wa Kimkakati Kamili (CSP), ambao mpango wake wa utekelezaji umeainishwa katika Mpango Mkakati wa Miaka Kumi wa Ushirikiano huo wa mwaka,(2020–2029).

Ziara ya Kiserikali ya Rais Xi ya tarehe 22 Agosti itawapa viongozi na wajumbe wao fursa ya kutafakari kuhusu maendeleo chini ya Ushirikiano wa Kimkakati na maendeleo pamoja na kuzingatia kuimarisha zaidi ushirikiano. Ambapo serikali hizo mbili zimekuwa zikishiriki katika utekelezaji wa miundo kama vile Tume ya Taifa Binafsi, Kikundi Kazi cha Pamoja, Utaratibu wa Kubadilishana Watu-kwa-Watu na Majadiliano ya Kimkakati.

Afrika Kusini na China zinafurahia uhusiano mzuri wa kiuchumi na China ndiyo mshirika mkubwa wa kibiashara wa kimataifa wa Afrika Kusini. China ni mwekezaji mkubwa nchini Afrika Kusini na inatoa msaada katika miradi ya maendeleo ya miundombinu ikiwa ni pamoja na Mradi wa Maendeleo ya Bandari Ndogo, Mradi wa Ukarabati wa TVET na Mradi wa Maji wa Mzimvubu, ambayo yote ni muhimu katika kuunda ajira. Majadiliano wakati wa Ziara ya Serikali yatachunguza ushirikiano zaidi na ubia ambao mataifa hayo mawili yanaweza kuimarisha uhusiano uliopo wa kidiplomasia, kiuchumi na kati ya watu na watu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.