Pamoja na Serikali kutoa bei elekezi ya Mbolea bado baadhi ya Wafanyabiashara wa Pembejeo wanauza bei ya juu ambapo mbolea ya Kupandia Shilingi 57,300 lakini wanauziwa 80,000 huku ya kukuzia ikiuzwa 60,000 badala ya 47,000 kama bei elekezi inavyoelekeza.
Wakulima wa Ikulwa wamelima hekari 1200 baada ya kuhamasishwa sana na Serikali. Mkoa wa Geita unawakutanisha Wafanyabiashara wa Pembejeo kwani Kutokana na Changamoto ya mbolea Serikali imeamu kutumia utaratibu wa kuingiza mbolea nchini chini ya mfumo wa ununuzi wa pamoja.
Utaratibu huu unatekelezwa kwa kuwa na bei elekezi katika kila Halmashauri kutegemeana na umbali kutoka Dar Es Salaam.
Katika Msimu wa 2017/2018 wakulima wa zao la pamba wameshalima zaidi ya hekta 80,000 ikilinganishwa na msimu wa 2016/2017 ambapo walilima hekta 24,000 ya kukuzia bei elekezi 47000 wanauziwa elf 60.
Picha na mtandao.