Star Tv

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano.

Timu ya matabibu walipata virusi walipotibu mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa, ambaye alihitaji upasuaji, na wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Fort Portal.

Kwa mujibu na waziri wa afya Dkt. Jane Ruth Aceng amesema Margaret Nabisubi, mwenye umri wa miaka 58, anakuwa mhudumu wa afya wa nne kufa kwa Ebola.

Mwanafunzi wa udaktari Mtanzania, ambaye alikuwa sehemu ya timu hiyo, alifariki dunia mwishoni mwa juma. 

Aidha kuliliripotiwa kuwa mshukiwa wa kifo cha Ebola ambaye ni mkunga katika wilaya ya Mubende, ambaye aliaga dunia kabla ya kupimwa.

Wahudumu wa afya walikuwa wameelezea wasiwasi wao juu ya kutokuwa na vifaa vya kujilinda vya kutosha katika siku za kwanza za kuzuka kwa janga hilo.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa kumekuwa na kesi 43 zilizothibitishwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo kutangazwa wiki mbili zilizopita, na kumi kati yao wamekufa.

Maafisa wa afya walisema wamefuatilia zaidi ya watu 800 wanaoshukiwa kuwa walikutana na wale ambao wameambukizwa ugonjwa huo.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.