Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimarisha udhibiti wa Rais Felix Tshisekedi serikalini
Serikali mpya ya muungano ina mawaziri 57 wakiwemo wanawake 14, huku 10 tu ndio kutoka Baraza la Mawaziri lililopita
Huu ni muungano mpya wa Rais Tshisekedi uliotangazwa tarehe 6 Disemba baada ya kuvunja ushirikiano wake na Rais wa zamani Joseph Kabila
Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde, ambaye aliteuliwa mwezi Februari, amemtaja mchumi Nicolas Kazadi kuwa Waziri wa Fedha, Mwanaharakati wa zamani wa asasi za kiraia
Read MoreCopyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.