Star Tv

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi ameiasa jamii kujitahidi kuongeza ibada mbalimbali ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kutoa sadaka kwa wingi hasa kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee, watotoyatima, wenyeulemavu na masikini ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (S.W).

Mama Mariam aliyasema hayo kwa nyakati tofauti alipowatembelea wazee wa Welezo na Sebleni pamoja na watoto yatima waliopo Kijiji cha SOS na Mazizini ,Mkoa wa Mjini Magharibi ambako aliwasalimia, kuwafariji na kuwapa zawadi ya futari pamoja na mabegi ya shule watotoyatima.

Amesema ibada ya sadaka sio lazima kutolewa zaidi kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, bali hata siku za kawaida kwani zinaogeza upendo na kuigusa jamii yenye uhitaji. “Kama kawaida desturi yetu mwezi wa Ramadhan huwa tunatembeleana, kujuliana hali, sio desturi pekee lakini pia ni maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, anatutaka waja wake kutoa sadaka kwa wingi na kufanya zaidi mambo mazuri ya kumridhisha Yeye kama kuwakumbuka wazee, wajane, watu wasiojiweza na masikini kuwapa sadaka ili nao watekeleza vizuri ibada hii ya mwezi mtukufu wa Ramandani” Alisema Mama Mariam. Miongoni mwa msaada waliopatiwa wazee na watoto hao ni pamoja na tende, vyakula vikiwemo mchele, unga wa ngano, sembe, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na vyakula vya nafaka.

CHANZO: IKULU ZANZIBAR

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.