Zaidi ya mataifa 25 na mashirika karibu 20 yamezindua muungano wa kimataifa wa kukabiliana na ukame, wakati wa mkutano wa kimataifa wa mazingira nchini Misri, chini ya uongozi wa Uhispania na Senegal.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pendro Sanchez amesema muungano huo utalenga kupambana na ukame popote utakapojitokeza, na kutangaza kuwa nchi yake itachangia kiasi cha awali cha dola milioni tano katika mwaka wa kwanza. Sanchez amesema Ulaya imeshudia ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 500 mwaka huu, na Afrika na maeneo mengine ya dunia pia yanakumbwa na uhaba mkubwa wa maji. Ameonya kuwa hakuna nchi moja itayoepuka madhara ya ukame, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono mkakati huo.
CHANZO: DW SWAHILI
Add a commentMapigano ‘makali’ kati ya wanajeshi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wasi wa M23 katika eneo la Rutshuru yameendelea kwa siku ya sita ambapo imethibitishwa kuwa eneo la Ntamugenga limetekwa na M23.
Add a commentPentagon na jumuiya ya kijasusi ya Marekani wamesema wanafuatilia harakati zozote za silaha za nyuklia nchini Urusi wakati wa mazoezi ambayo maafisa wa Marekani wanasema yanapaswa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi.
Add a commentRishi Sunak sasa atachukua nafasi ya Waziri Mkuu katika wakati mgumu sana kwa uchumi wa taifa hilo, Ambapo bado haijasikika mipango yoyote ya kina kutoka kwake tangu kampeni ya uongozi katika msimu wa joto.
Add a commentMaelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa Tunisia kuandamana dhidi ya Rais wa nchi hiyo.
Add a commentWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum [ ... ]
Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]
Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.