Star Tv

Maafisa wa utawala nchini Tanzania wamesema kuwa hawatawafungulia mashtaka wasichana watano wa shule waliopata ujauzito ambao walikamatwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya mkuu wa wilaya kuagiza kukamatwa kwao.

Hatua hiyo iliibua mjadala mkali huku wanaharakati wa kijamii wakipinga hatua hiyo ya serikali wakisema kuwa agizo hilo inakandamiza haki za watoto hao.

Wanaharakati wanaohusika na utetezi wa haki za watoto na wanasema uamuzi wa kuwakamata wazazi hauwezi kuwa njia pekee ya kutokomeza mimba za utotoni bali serikali inapaswa pia kuangazia visababishi vingine vinavyochangia ongezeko la mimba za utotoni.

Edison Sosten, ni afisa katika shirika la kupigania haki za wanawake Tanzania, TAMWA anasema kuwa "Kuna vikwazo vingi ambavyo mabinti wanakutana navyo na sio tu ya nyumbani, japo analelewa na mzazi, bado anakutana na vishawishi vingi akiwa anatoka shuleni".

 

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byankwa alisema kwamba maamuzi hayo yanalenga sio kuwaadhibu wazazi bali kujenga ushirikiano nao, kwa sababu wengi wamekuwa wakificha majina ya watu waliowapatia mimba watoto kwa sababu ya kufahamiana nao.

Kwa mujibu wa shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch, nchini Tanzania zaidi ya watoto 15,000 hukatisha masomo yao kila mwaka kutokana na mimba za utotoni na kwa mujibu ya utafiti wa afya ulioganywa na wizara ya afya mwaka 2015 hadi 2016 , asilimia 27 ya watoto wa kike wamepata watoto wakiwa kati ya miaka 15 na 19.

Mwaka jana, Agosti, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitoa marufuku kwa wasichana wanaopata ujauzito kuendelea na masomo katika shule za serikali.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.