Pentagon na jumuiya ya kijasusi ya Marekani wamesema wanafuatilia harakati zozote za silaha za nyuklia nchini Urusi wakati wa mazoezi ambayo maafisa wa Marekani wanasema yanapaswa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi.
Afisa mkuu wa Pentagon aliiambia CNN kwamba matamshi ya nyuklia ya Urusi na uamuzi wa kufanya mazoezi katikati ya vita na Ukraine ni kutowajibika.
Kwa mujibu wa Marekani, mazoezi hayo ya Urusi hufanyika kila mwaka na, huku Baraza la Usalama la Taifa la Marekani nalo limesema vikosi vyake vitaanza mazoezi hayo kivyake ambayo yatajumuisha kurusha makombora ya moja kwa moja na kupelekwa kwa vifaa vya kimkakati.
Kwa upande wake, NATO imebainisha kuwa itaanza Jumatatu hii mazoezi yake ya kila mwaka ya nyuklia, ambayo yatahudhuriwa na nchi 14, pamoja na Marekani.
#ChanzoBBC