Star Tv

Makamu wa Rais wa Marekani Bi, Kamala Harris, amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dk, Philipo Mpango.

Hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea nchini hapa, ambaye ameambatana na mumewe kwa mualiko maalum kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu. Makamu wa Rais Kamala atakuwa na ziara ya Siku tatu.

Huku Marekani imekuwa ni mshirika mkubwa wa maendeleo na pia atakuwa na mazungumzo na Rais Dk; Samia Suluhu, lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya pande mbili hali kadhalika mengine yanayotarajiwa kuongelewa ni pamoja na suala la maendeleo ya uchumi, mabadiliko ya Tabia nchi, usalama wa chakula pamoja na maendeleo ya demokrasia na mengineyo ambayo ni ajenda kuu katika ziara yake hii nchini Tanzania. Vile vile atapata nafasi ya kukutana na wasanii wa Tanzania katika na kuongelea juu ya kazi zao na ushirikiano baina ya mataifa haya. Ikiwa ni muunganiko wa ziara anazofanya Africa ambapo ameanzia ziara yake nchini Ghana, kisha atamalizia nchini Zambia.

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.