Rishi Sunak sasa atachukua nafasi ya Waziri Mkuu katika wakati mgumu sana kwa uchumi wa taifa hilo, Ambapo bado haijasikika mipango yoyote ya kina kutoka kwake tangu kampeni ya uongozi katika msimu wa joto.
Rishi Sunak amepanda jukwaani kwa hotuba yake ya kwanza kwa umma kama kiongozi wa Tory ambapo ametoa pongezi kwa Liz Truss kwa uongozi wake "wenye heshima" "chini ya hali ngumu nje ya nchi na nyumbani".
Sunak ameahidi kutumikia kwa uadilifu na unyenyekevu nafasi hiyo ya Uwaziri Mkuu, "nitafanya kazi siku baada ya siku kwa ajili ya watu wa Uingereza. Ninaahidi kuwa nitahudumu kwa uadilifu na unyenyekevu," Sunak alisema.
Rishi Sunak amesema Uingereza ni nchi kubwa lakini inakabiliwa na changamoto "kubwa" za kiuchumi.
Wiki saba baada ya kushindwa katika uchaguzi wa viongozi wa Conservative, Rishi Sunak sasa atakabidhiwa ufunguo wa Downing Street.
Sunak ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Uingereza mwenye asili ya Asia, na atachukua madaraka huku Uingereza ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi.