Star Tv

Baada kufanikiwa kupata ushindi wa ugenini na nyumbani katika michezo miwili ya ligi ya mabingwa Africa baadhi ya wadau wa soka wameuomba uongozi wa klabu ya Simba kuendelea kumuamini kocha wao wa muda Juma Mgunda.

Wadau mbalimbali wa soka wameongea juu ya suala hili, akiwemo Mchezaji wa zamani wa timu ya Kariakoo ya Lindi na mchambuzi wa soka Jemedari Said amesema uongozi wa klabu ya Simba unatakiwa kuendelea kumuamini Mgunda kutokana na mabadiliko ya kiuchezaji aliyoyafanya kwenye timu hiyo. Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema wataendelea kuwa na kocha wao wa muda hadi pale uongozi wa klabu hiyo utakapotoa taarifa ya mabadiliko ya benchi la ufundi. Kocha wa muda wa klabu ya Simba Juma Mgunda ameiongoza timu hiyo katika michezo mitatu, mmoja wa ligi na miwili ya ligi ya mabingwa ambayo ameshinda michezo yote na kufunga mabao matano.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.