Star Tv

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum cha kufanya ufuatiliaji wa magonjwa hasa ya mlipuko ili kuyapatia udhibiti wa uharaka zaidi.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku nne kwa watoa huduma za afya mkoa wa Dar es salaam yanayolenga kuwajengea uwezo wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola ambao bado haujathibitika kuwepo nchini. "Amesema kupitia takwimu za Ugonjwa wa ebola nchini Uganda hadi sasa kesi za wagonjwa 132 zimeripotiwa huku idadi ya watumishi wa afya wakiwa 18 kati yao 7 wamefariki, hali inayoilazimu wizara ya afya ya Tanzania kutoa mafunzo hayo kwa wataalumu wake". Amesema Serikali itaendelea kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kwa makundi mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waganga wa jadi.

Ambapo, mafunzo hayo ya siku nne yatatolewa kwa Halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es salaam na kuwafikia watumishi wa afya 3757 kutoka vituo mbalimbali vya afya mkoani humo.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.