Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Serikali ya Marekani kufanya marejeo ya mkataba wa Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (African Growth and Opportunity Act - AGOA) na kuuhuisha hadi mwaka 2030.

Rais Samia ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumpokea mgeni wake Mhe. Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani ambae yuko katika ziara ya kikazi nchini. Aidha, Rais Samia amesema mpango wa AGOA ambao unaisha mwaka 2025 ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa ni njia pekee ya biashara ambayo bara la Afrika linautegemea kujikomboa kutoka lindi la umaskini. Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa Marekani kufanya mapitio ya Mkataba wa Viza ili kuwawezesha raia wa mataifa yote mawili kunufaika na viza ya muda mrefu kwa kuongeza ukuaji wa biashara, utalii na uwekezaji.

Rais Samia pia ameishukuru Marekani kwa msaada wanaoutoa katika kuleta maendeleo nchini kwenye sekta za afya, elimu, maji, usafi wa mazingira, kilimo na usalama wa chakula, maliasili, maendeleo ya miundombinu, demokrasia, pamoja na utawala bora. Rais Samia amesema ziara ya Mhe. Harris itatoa fursa kwa nchi hizi mbili kuimarisha mahusiano yaliyopo na kuwa jukwaa la kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano zaidi. Kwa upande wake, Mhe. Harris amemtaja Rais Samia kama kiongozi bingwa wa mageuzi ambapo pia amesisitiza nchi hizi zitaendelea na majadiliano juu ya ukuaji wa uchumi wa muda mrefu nchi Tanzania.

Chanzo: Ikulu Mawasiliano.

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.