Star Tv

Klabu ya Real Madrid imeendeleza rekodi yake ya ushindi msimu huu baada ya kuifunga klabu ya Atletico Madrid katika mchezo wa Derby ya jiji la Madrid.

Ushindi huo umeifanya klabu hiyo iendelee kubaki nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo iki fuatiwa na mahasimu wao Barcelona huku ikiwa imeweza kushinda mechi zote sita za mwanzoni mwa msimu huu. Klabu hiyo inayonolewa na Carlo Ancelotti imeweza kurudia rekodi yake ya kushinda mechi zote sita za mwanzoni mwa msimu ambapo kwa mara ya mwisho ilifanya hivyo msimu wa mwaka 1987-88. kwa upande mwingine mechi hiyo ilitawaliwa na nyimbo zilizoonekana kuwa za kibaguzi zinazomlenga mchezaji wa Madrid Vinicius Jr zikikosoa aina yake ya ushangiliaji baada ya kufunga goli pia baadhi ya mashabiki walimtupia uchafu mchezaji huyo.

Latest News

MUHUDUMU MWINGINE AFARIKI KWA EBOLA UGANDA.
05 Oct 2022 12:44 - Grace Melleor

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kifo cha mhudumu mwingine wa afya, ambaye amefariki alfajiri ya leo Jumatano. [ ... ]

KIONGOZI MKUU WA IRAN AILAUMU MAREKANI NA ISRAEL.
04 Oct 2022 14:14 - Grace Melleor

Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mw [ ... ]

WAHITIMU 1,384,340 KUANZA MTIHANI.
04 Oct 2022 13:56 - Grace Melleor

Jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika Oktoba tano na sita  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.