Star Tv

China inadaiwa kuwa itafungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti.

Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika.

"Badala ya kushirikiana na serikali za mataifa hayo, [China] imeamua…kushirikiana na United Front linked, mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu"- Watetezi hao wa usalama walisema.

Waliongeza kuwa mamlaka ya China, kati ya Aprili 2021 na Julai 2022, "imewashawishi" raia 230,000 kurejea China kujibu mashtaka ya jinai kuhusu mawasiliano ya simu na ulaghai wa jumla.

Serikali ya China ilipiga marufuku raia wake kuhamia nchi tisa ambazo hazikutajwa kwa makosa ya "udanganyifu mkubwa, ulaghai wa simu na uhalifu wa mtandao".

#ChanzoBBC

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.