Star Tv

Zaidi ya mataifa 25 na mashirika karibu 20 yamezindua muungano wa kimataifa wa kukabiliana na ukame, wakati wa mkutano wa kimataifa wa mazingira nchini Misri, chini ya uongozi wa Uhispania na Senegal.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pendro Sanchez amesema muungano huo utalenga kupambana na ukame popote utakapojitokeza, na kutangaza kuwa nchi yake itachangia kiasi cha awali cha dola milioni tano katika mwaka wa kwanza. Sanchez amesema Ulaya imeshudia ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 500 mwaka huu, na Afrika na maeneo mengine ya dunia pia yanakumbwa na uhaba mkubwa wa maji. Ameonya kuwa hakuna nchi moja itayoepuka madhara ya ukame, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono mkakati huo.

 

CHANZO: DW SWAHILI

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.