Star Tv

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeitisha kikao cha dharura hii leo kujadiliana hali ya kisiasa na usalama nchini Sudan.

Jeshi la Sudan na kikosi maalumu cha wanamgambo cha Rapid Support Forces, RSF wameendelea kwa siku ya pili kupambania udhibiti wa taifa hilo, hali inayoashiria kutokuwa tayari kumaliza uhasama licha ya kuongezeka kwa shinikizo la kidiplomasia la kusitisha mapigano.

Mapigano makali ya ardhini na angani yameshuhudiwa hii leo katika mji mkuu, Khartoum na mji unaopakana nao wa Omdurman pamoja na maeneo mengine yanayozozaniwa nchini humo. Kulingana na Kamati Kuu ya madaktari nchini Sudan, watu 56 wameuawa ikiwa ni pamoja na watumishi watatu wa shirika la Mpango wa chakula ulimwenguni, WFP. Shirika hilo limetangaza kusitisha kwa muda shughuli zake nchini humo. Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya watumishi hao waliokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeitisha kikao cha dharura hii leo kujadiliana hali ya kisiasa na usalama nchini Sudan, hii ikiwa ni kulingana na taarifa kupitia ukurasa wa Twitter. Katika hatua nyingine, Misri kupitia mwakilishi wake kwenye Muungano wa mataifa ya Kiarabu, imezitaka pande zinazohasimiana kuhakikisha usalama wa maslahi yake.

CHANZO: DW KISWAHILI

Latest News

Dkt. Jafo ofisi yake, imekamilisha taratibu zote za kupata Ithibati ya Kitabu ch...
24 Apr 2023 09:38 - Kisali Shombe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha bungeni Hotuba ya Ma [ ... ]

TARI, Ukiruguru kuzindua Kifaa cha kupandia Mbegu cha Rafiki
23 Apr 2023 18:33 - Kisali Shombe

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa uj [ ... ]

Wanawake kuwa sehemu ya Elimu dhidi ya Itikadi Kali na Ugaidi Afrika.
17 Apr 2023 10:28 - Kisali Shombe

Mnamo Oktoba 14, 2017, Mogadishu, Somalia ilikumbwa na shambulio baya la kigaidi lililoua watu 587 na kujeruhi zaidi ya  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.