Star Tv

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa baada ya kufariki Rais wa pili wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi.

Add a comment

Rais Dokta John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali leo Februari 03,2020 ambao  aliwateua hivi karibuni.

Add a comment

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan nchini China kwa ujumla kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa ya Corona nchini humo.

Habari na Angela Mathayo.

Add a comment

Leo tarehe 29/01 katika Bunge la 11 kikao cha pili, hati zilizowasilishwa mezani ni pamoja na taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2019 ambazo zitawasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali. Vile vile uwasilishwaji wa taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa kuhusu usimamizi wa matumizi ya fedha za umma katika serikali za mitaa kwa mwaka 2019,ambazo zitawasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa.

Add a comment

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera umeieleza Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa mchakato wa makubaliano kati ya Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) bado unaendelea.

Habari na Angela Mathayo.

Add a comment

Bunge la 11 mkutano wa 18 limeanza leo tarehe 28/1/2020, bunge hili ni mahususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za mwaka za kamati za kudumu za Bunge., ambapo Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na. 5), wa mwaka 2019, na muswada wa sheria ya ususluhishi wa mwaka 2020.

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria  itakayofanyika katika Jiji la Dodoma.

Add a comment

Wanafunzi zaidi ya 2700 wa shule ya msingi Bangulo iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam wanalazimika kutumia matundu ya vyoo nane tu hali inayotajwa kuwapa shida wanafunzi hao wakati wanapohitaji kujisaidia huku shule hiyo ikiwa na jumla la madarasa 14 pekee ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi  shuleni hapo

Habari na Adam Damian.

Add a comment

Mpango wa utoaji chakula shuleni mkoani Geita bado uko chini ambapo takwimu zinaonyesha kuwa  shule za msingi zilizopo ni 598 na  zinazotoa chakula ni 143 sawa na asilimia 23.9 huku inaelezwa kuwa  baadhi ya wazazi bado wanaona hakuna umuhimu wa kuchangia chakula kwakuwa serikali ilishatoa  tamko yakuwa Elimu bure kwa kila mwanafunzi.

Habari na Salma Mrisho.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.