Star Tv

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo na hali za watanzania wanaoishi jimboni Wuhan nchini China kwa ujumla kutokana na kuzuka kwa virusi vya homa ya Corona nchini humo.

Habari na Angela Mathayo.

Prof. Kabudi amesema Tanzania ina wanafunzi takribani 4000 ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 ambapo kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Mbelwa Kairuki ameihakikishia serikali kuwa mpaka sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.

Prof Kabudi amewataka watanzania kuwa watulivu na kupenda kuwa na subira ya kupata maelezo na ufafanuzi rasmi kutoka kwa Serikali pale panakotokea jambo badala ya kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii na  nakuamini habari hizo za uvumi kwani kwa kufuatilia habari hizo kutoka vyanzo husika vya kutoa habari kutaondoa uenezi wa habari zinazoua  taharuki.

Aidha amewataka watanzania kuwa makini na suala la kutoa taarifa zisizo rasmi ama uvumi ambazo hazijathibitishwa kutoka kwa mamlaka husika  kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tanzania na amewasihi wawe na subira wakati wakiendelea  kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.

                                                                                                               Mwisho

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.