Star Tv

Bunge la 11 mkutano wa 18 limeanza leo tarehe 28/1/2020, bunge hili ni mahususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za mwaka za kamati za kudumu za Bunge., ambapo Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na. 5), wa mwaka 2019, na muswada wa sheria ya ususluhishi wa mwaka 2020.

Hali kadhalika ni pamoja na kushughulikia hoja mbalimbali za ukaguzi kama zilivyoripotiwa katika taarifa ya hesabu zilizokaguliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha wa 2018.

Vile vile kufanya uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasirishwa wakati wa mkutano wa 17. 

 

Baadhi ya maswali ambayo yamewasilishwa na kuomba kupatiwa majibu na serikali ni pamoja na swali lililoulizwa na

Mheshimiwa Dkt.Sulemani Ally Yussuf (Mgogoni)

Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kumekuwa na ongezeko kubwa la makosa katika Jamii jambo ambalo linasababisha mfumo wa utoaji haki pamoja na Mahakama kuelemewa

(a) Je kila Jaji au Hakimu anapangiwa kesi ngapi kwa mwaka ili kupunguza mlundikano wa kesi

(b) Je, ni mambo gani kimsingi yanayosababisha mashauri kuchukua muda mrefu.

Vilevile Mheshimiwa Ruth Hiyob Mollel (Viti Maalum),Ameuliza juu ya

Shule ya Msingi Vikindu katika Wilaya ya Mkuranga ina mikondo miwili (A na B) darasa la kwanza hadi la Saba, na mwaka 2019 Darasa la kwanza na la Pili yalikuwa na wanafunzi 300 kila Darasa;-

(a) Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha uwiano wa Mwalimu na Mwanafunzi wa 1:45 unazingatiwa kwa mujibu wa sera ya elimu ya msingi;

(b) Je, kwa msongamano huo tunaweza kupata wanafunzi walioelimika na kukidhi malengo ya Tanzania ya viwanda.

 Hali Kadhalika Mheshimiwa Tunza Issa Malapo (Viti Maalum) ameuliza

Je ni lini Serikali itapeleka X-Ray machine mpya katika Hospitali ya Rufaa ya Mtwara – Ligula?

Mheshimiwa Sikudhani Yasini Chikambo (Viti Maalum) ameuliza;

Kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wa mtaani ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia watoto hao.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.