Star Tv

Mpango wa utoaji chakula shuleni mkoani Geita bado uko chini ambapo takwimu zinaonyesha kuwa  shule za msingi zilizopo ni 598 na  zinazotoa chakula ni 143 sawa na asilimia 23.9 huku inaelezwa kuwa  baadhi ya wazazi bado wanaona hakuna umuhimu wa kuchangia chakula kwakuwa serikali ilishatoa  tamko yakuwa Elimu bure kwa kila mwanafunzi.

Habari na Salma Mrisho.

Halmashauri ya mji  wa Geita ina  shule za msingi 51 ikiwa na idadi ya Wanafunzi 68,386 suala la utoaji chakula limeonyesha kupewa kipaumbele kwa shule nyingi ingawa hali halisi inayoshuhudiwa ni  suala lenye kuleta ugumu katika utekelezaji wake.

Shule ya msingi Kasamwa ambayo imewakutanisha wazazi katika kikao mambao moja ya agenda zao ni kujadili suala la chakula ambao wanasema hali ya kipato ndiyo inawafanya baadhi ya wazazi wengine kushindwa kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya watoto kupata chakula.

Inaelezwa kuwa wazazi wenye watoto watano na kuendelea wanakutana na changamoto kubwa ya kuweza kuwalipia watoto wote fedha kwa ajili ya chakula na shule kwa mwezi mzazi anatakiwa kuchangia shilingi 2750 tu.

Baadhi ya wazazi wanaelezwa kuwa tabia ya kutohudhuria vikao vya shule kila mara wanapoitwa na inaelezwa kuwa wazazi hao ndio hawajachangii suala la chakula lakini jambo hilo bado haliwakatishi tamaa wazazi wa wanafunzi wachache kuendelea kuchangia.

Shule ya Msingi Kasamwa ilianza utoaji wa uji novemba 2019 ambapo idadi ya watoto waliokuwa wamechanga na kupata uji ni 200 na mwaka huu 2020 ni 112 na uongozi wa shule unasema huenda imani uchangiaji ikazidi kuendelea.

Kimkoa hali hiyo ya utoaji chakula kwa wilaya ya Bukombe ni asilimia sifuri, Chato 41.4%, Geita Mji 19.6,Wilaya ya Geita ni 2.6%, Mbogwe 52.3% na Nyang’wale 48.4.

                                                                                                                                    Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.