Star Tv

Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU imefuta hati za usajili wa vyuo vikuu vishiriki vitano, vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu kishiriki kimoja baada ya kushindwa kufanya maboresho waliyopewa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Taarifa zaidi na Angella Mathayo.

Hayo yamesemwa na katibu mtendaji wa TCU  Profesa Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa vyuo hivyo vimeshindwa kujirekebisha na hata vingepewa muda zaidi visingeweza.

Katika hatua nyingine TCU imefuta hati za usajili za vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu kishiriki kimoja baada ya baada ya kushindwa kufanya maboresho kwa muda waliopewa ikiwa ni pamoja na uhaba wa rasilimali fedha katika kujiendesha.

TCU imerejesha udahili wa wanafunzi wapya katika chuo kikuu kishiriki cha afya na sayansi shirikishi cha Mt. Fransisko baaada ya kurekebisha mapungufu yaliyokuwepo.

Aidha, TCU imesitisha udahili wa wanafunzi wapya wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa ambapo chuo hicho kimepewa miezi sita  kuweza kukamilisha utekelezaji wa maelekezo ya tume.

                                                                                        Mwisho

Latest News

KUNDI LA MAI-MAI LAENDELEA KUUTESA MJI WA LUBUMBASHI KWA MAPIGANO.
26 Sep 2020 15:30 - Grace Melleor

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mku [ ... ]

AJALI YA NDEGE YA JESHI LA UKRAINE YASABABISHA VIFO VYA WATU 22.
26 Sep 2020 08:31 - Grace Melleor

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa na abiria watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. [ ... ]

BAH N'DAW KUAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO NCHINI MALI.
25 Sep 2020 09:24 - Grace Melleor

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.