Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro kimeandaa mpango maalumu utakaowawezesha wahitimu wake katika chuo hicho kuweza kujiajiri na kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo.
Habari na Peter Laurence..........
Uwepo wa idadi kubwa ya wahitimu wanaomaliza elimu ya juu nchini inatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajira na hivyo kupelekea vijana wengi kukosa ajira na kubaki kulalama.
Ukosefu wa misingi bora kwa wanafunzi wa elimu ya juu kunatajwa kuwa ndio chanzo cha kushindwa kujiajiri kwa wahitmu wengi na hivyo mpango huo unasimamiwa na kitengo cha huduma za ajira chuoni hapo TESCEA kutajwa kuwa ndio dawa ya changamoto hiyo.
Aidha, mpango mkakati uliopo kwa sasa ni kuanza kufundishwa kwa somo la ujasiriamali vyuoni ili kuweza kupunguza changamoto ya ajira kwa wahitimu.
Ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana ndio changamoto inayobainishwa na baadhi ya wanafunzi kuwapelekea katika msukosuko wakukosa ajira na kushindwa kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao ya elimu ya juu..
Baada ya miaka kadhaa ijayo mpango huo unatarajia kuleta majibu chanya kwa kuonyesha idadi ya wahitimu waliojiajiri huku uwajibikaji na ufanisi kwa wanafunzi hao ukitajwa kuchochea mafanikio ya mpango huo na kuweza kupunguza changamoto ya ajira.
Mwisho