Mpango wa utoaji chakula shuleni mkoani Geita bado uko chini ambapo takwimu zinaonyesha kuwa shule za msingi zilizopo ni 598 na zinazotoa chakula ni 143 sawa na asilimia 23.9 huku inaelezwa kuwa baadhi ya wazazi bado wanaona hakuna umuhimu wa kuchangia chakula kwakuwa serikali ilishatoa tamko yakuwa Elimu bure kwa kila mwanafunzi.
Habari na Salma Mrisho.
Halmashauri ya mji wa Geita ina shule za msingi 51 ikiwa na idadi ya Wanafunzi 68,386 suala la utoaji chakula limeonyesha kupewa kipaumbele kwa shule nyingi ingawa hali halisi inayoshuhudiwa ni suala lenye kuleta ugumu katika utekelezaji wake.
Shule ya msingi Kasamwa ambayo imewakutanisha wazazi katika kikao mambao moja ya agenda zao ni kujadili suala la chakula ambao wanasema hali ya kipato ndiyo inawafanya baadhi ya wazazi wengine kushindwa kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya watoto kupata chakula.
Inaelezwa kuwa wazazi wenye watoto watano na kuendelea wanakutana na changamoto kubwa ya kuweza kuwalipia watoto wote fedha kwa ajili ya chakula na shule kwa mwezi mzazi anatakiwa kuchangia shilingi 2750 tu.
Baadhi ya wazazi wanaelezwa kuwa tabia ya kutohudhuria vikao vya shule kila mara wanapoitwa na inaelezwa kuwa wazazi hao ndio hawajachangii suala la chakula lakini jambo hilo bado haliwakatishi tamaa wazazi wa wanafunzi wachache kuendelea kuchangia.
Shule ya Msingi Kasamwa ilianza utoaji wa uji novemba 2019 ambapo idadi ya watoto waliokuwa wamechanga na kupata uji ni 200 na mwaka huu 2020 ni 112 na uongozi wa shule unasema huenda imani uchangiaji ikazidi kuendelea.
Kimkoa hali hiyo ya utoaji chakula kwa wilaya ya Bukombe ni asilimia sifuri, Chato 41.4%, Geita Mji 19.6,Wilaya ya Geita ni 2.6%, Mbogwe 52.3% na Nyang’wale 48.4.
Mwisho.