Jeshi la kuhifadhi wanyapori TANAPA hifadhi ya Taifa Katavi Kanda ya Kusini kwa kushirikina na jeshi la polisi mkoani Rukwa limefanikiwa kuwakamata watu wanne ambao walitaka kutorosha na kusafirisha meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja thelathini na saba za kitanzania katika kijiji cha Saafu wilayani Kalambao mkoani Rukwa.
Habari na Brown Lawi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habri Kamishina Mwandamizi TANAPA Kanda ya kusini Christofa Timbuka amesema kukamatwa kwa wahalifu hao kunatokana na ushirikiano kati ya TANAPA ,raia wema na vyonmbo vingine vya ulinzi na usalama
Kamishina Mwandamizi wa TANAPA Kanda ya Kusini ameitaka jamiii kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukomesha vitendo hivyo vya ujangili .
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho cha Saafu wakioneshwa kusikitishwa na matendo ya ujangili wanasema suala la ujangili linapaswa kukemewa vikali ili kukomeshwa kwakuwa lipoteza pato la taifa na vitendo hivyo vinaharibu shughuli za utalii pamoja nakuikosesha serikali fedha za kigeni.
Mwisho.