Star Tv

Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Njombe imeendelea kusikiliza kesi inayomkabili Mwalimu Focus Mbilinyi anayekabiliwa na tuhuma za kumpiga mwanafunzi na kumsababishia.

Habari Zaidi na Dickson Kanyika

Shauri hilo namba 141 la mwaka 2019 linaloendeshwa na Hakimu Ivran Msaki mbele ya mawakili wasomi Elizabeth Malya upande wa serikali huku upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili Octavian Mbugwani , Innocent Kibadu na Lilian Gama limeendelea kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa njombe.

Mahakama imewasikiliza mashahidi wawili wa upande wa utetezi ambao wote wameiambia mahakama kwamba Hosea alipigwa viboko vitatu sehemu za makalio kwa kosa la kutofanya hesabu alizopewa na mwalimu wake.

Mmoja wa mashahidi hao Sefania Kyelula ameiambia mahakama kwamba siku ya tarehe 21 mwezi machi mwaka 2017 Hosea Manga alipowasili shuleni alimueleza kwamba alikuwa akisumbuliwa na miguu kabla ya kupigwa na kusababishiwa ulemavu.

Mashahidi wote wawili wameiambia mahakama kwamba Hosea Manga hakuning’inizwa dirishani kama ilivyoelezwa hapo awali na mashahidi wa upande wa jamhuri.

Mwalimu Focus Mbilinyi anadaiwa kumpiga mwanafunzi Hosea na kumsababishia ulemavu siku ya tarehe 21 mwezi machi  mwaka 2017.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi tarehe 4 mwezi February mwaka huu itakaposikilizwa tena kwa ajili ya majumuisho na kutajwa tarehe ya hukumu.

                                                                                 Mwisho.

 

 

Latest News

KUNDI LA MAI-MAI LAENDELEA KUUTESA MJI WA LUBUMBASHI KWA MAPIGANO.
26 Sep 2020 15:30 - Grace Melleor

Mapigano yametokea kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mku [ ... ]

AJALI YA NDEGE YA JESHI LA UKRAINE YASABABISHA VIFO VYA WATU 22.
26 Sep 2020 08:31 - Grace Melleor

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa na abiria watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. [ ... ]

BAH N'DAW KUAPISHWA KUWA RAIS WA MPITO NCHINI MALI.
25 Sep 2020 09:24 - Grace Melleor

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.