Star Tv

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera umeieleza Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa mchakato wa makubaliano kati ya Kabendera na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) bado unaendelea.

Habari na Angela Mathayo.

Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Janet Mtega kuwa majadiliano kati ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP) na mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera bado unaendelea.

Mwenda amesema kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Katika maelezo yake, Mwenda amesema kuwa majadiliano kati ya mshtakiwa na DPP bado yanaendelea, kuiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 10 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.

Kwa mara ya kwanza Kabendera alifikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019 akikabiliwa na makosa hayo anayodaiwa kuyafanya kati ya Januari 2015 na Julai 2019, jijini Dar es Salaam.

                                                                                Mwisho

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.