Star Tv

Maafisa usafirishaji na wafanya biashara wadogo wa kituo cha mabasi Halmashauri ya mji wa Makambako wameiomba halmashauri kuchukua hatua za haraka kufanya ukarabati wa Kituo hicho, ili kuepusha hasara na mlipuko wa magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na ubovu wa miundombinu ya kituo hicho.

Taarifa na Dickson Kanyika

Add a comment

Naibu waziri  wa Nchi  Ofisi ya Rais  TAMISEMI Mwita Waitara amemwagiza Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamkamata Chacha Magitha  Mkazi wa Kebikiri Mjini Tarime kwa tuhuma za kuuza eneo la Umma kinyume na Taratibu.

Add a comment

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein amewataka mawaziri wanaoshiriki mkutano wa kwanza wa SADC kuhakikisha wanapitisha mikakati imara itakayoweza kuondoa ama kupunguza madhara ya majanga.

Taarifa na Abdalla Pandu.

Add a comment

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi wa Polisi Mugabo Wekwe kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa vituo vya Pangawe na Kingolwira.

Add a comment

 

Baadhi ya waumini wa kanisa la  Anglikana Dayosisi ya Zanzibar  wamesema hawana imani na uongozi wa Askofu wao Michael Hafidh kwa kile walichodai kuwa matendo yake  hayaendani na sifa za cheo alichonachoikiwemo suala la  ubadhrifu .

Taarifa na Abdalla Pandu-Zanzibar.

Add a comment

Polisi Mkoani Morogoro wamegundua mfumo mpya unaotumika kusafirisha  madawa ya kulevya kwa njia ya pikipiki na tayari watu wanne wanashikiliwa na polisi kwa kosa hilo.

Taarifa na Peter Laurence

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa ahadi ya kuwaajiri madaktari 1000 katika vituo vya afya pamoja na hospitali zilizopo nchini.

Add a comment

Upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu umeomba muda wa kutosha kupitia na kujibu maombi ya kujitoa kwa wadhamini wa makamu mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Taarifa na Angela Mathayo.

Add a comment

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya awamu ya saba itakamilisha ujenzi wa kiwanda cha Mwani kisiwani Pemba kama ilivyowaahidi wananchi wake.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.