Star Tv

 

Muamko wa Jamii katika uchangiaji wa damu salama umezidi kukua hali ambayo imesaidia kuokoa maisha ya Wagonjwa wenye uhitaji wa Damu hasa wakinamama wajawaziito na Watoto chini ya umri wa miaka 5 Mkoani Geita, ambapo ukiangalia mwaka 2018  damu iliyokusanywa ni chupa 12,393 sawa na asilimia 62 ukilinganisha mwaka 2017 chupa 5991 sawa na asilimia 34.

Add a comment

Kufuatia  migogoro  kushamiri kati ya wachimbaji wadogo na uongozi wa kitengo cha ukaguzi na usalama wa mgodi wa Ikuzi wilayani Bukombe ambapo Mkuu wa Wilaya  hiyo  Ndugu, Said Nkumba alitoa siku tatu kuhakikisha  Bodi ya ushirika inamuondoa  Inspekta mkuu ndugu, Said Manumbu anayelalamikiwa  kwa Rushwa ,Bodi ya Ushirika imetengua uongozi wote na kuchangua  viongozi wapya kutekeleza Agizo la Mkuu wa Wilaya.

Add a comment

MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara Charles Kabeho ameongoza zoezi la kuteketeza zao haramu la bangi kavu yenye uzito wa kg 2212 kwa moto iliyo kamatwa na  polisi Tarime Rorya katika kipindi cha miezi saba wakati wa oparesheni tokomeza madawa ya kulevya inayo endelea katika mkoa huo.

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Machi, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mhe. Sheikh Mohammed bin Abdulrahman J.A. Al Thani, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Add a comment

Hatimaye Wananchi wa Kijiji cha nyakafuro wakubali kuupokea Mwili wa Marehemu Jackson Charles anayedaiwa kusababishiwa kifo kutokana na kipigo cha polisi  baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga kuingilia kati mgogoro huo na kuwaahidi kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kama kuna makosa hatua za kisheria zitachukuliwa.

Add a comment

Migogoro ya Adhi katika baadhi ya maeneo hapa nchini imendelea kushamiri licha ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa Amani ambapo wananchi wa wa Kata ya Majengo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamemwomba Waziri wa Ardhi kuingilia kati Mgogoro wa Mipaka unaoendelea baina ya Kata Mbili za  Majengo na Makiba zilizopo kwenye Tarafa ya Mbuguni.

Add a comment

Tanzaniani ni miongozi mwa  nchi  12 za Bara la Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotekeleza mradi wa LDFS  lakini bado zinakabiliwa na  uharibifu wa Ardhi ,uwepo wa nusu jangwa, ikolojia iliyobaribika na uzalishaji duni wa chakula kutokana na uharibifu wa mazingara unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa mkaa  na kuharibu vyanzo vya maji.

Add a comment

 

Idara ya uhamiaji mkoani Mara imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 196 toka katika nchi za Afrika ya Kati wakivushwa na kuingizwa nchini kinyume cha sheria na wafanyabiashara wanaofanya biashara za binaadamu waliopo katika mpaka wa Sirali nchini Tanzania na Isibania Nchini Kenya.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.