Star Tv

Shirika la umeme nchini Tanesco Kanda ya Dar es salaam limefanya ukaguzi wa akaunti za luku eneo la Mchikichini wilaya ya Ilala na kubaini upotevu mkubwa wa umeme kutokana na wizi unaofanywa na baadhi ya wananchi na kusababisha shirika hilo kupata hasara.

Add a comment

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (mb) akizungumza na Wamiliki na viongozi wa vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. 

Add a comment

Shirika la World Vision kanda ya Kagera limekamilisha ujenzi wa matundu nane ya vyoo,madarasa matatu ya shule hiyo , ofisi ya walimu pamoja na wodi ya mama na Mtoto katika zahanati ya kijiji cha Kiruruma kwa jumla ya thamani ya shilingi milioni mia moja sitini na tisa na kuzinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka huku meneja mradi wa World Vision.

Add a comment

Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA) Juni nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao, na wanyama walao nyama  na uwepo wa ukanda mrefu wenye wanyama wengi imepangwa kukabidhiwa kwa raisi Dkt John Magufuli.

Add a comment

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas ameongoza operesheni katika Wilaya ya Kibiti, Kijiji cha Rungungu eneo ambalo mauaji yalilindima na kutikisa Mkoa wa Kipolisi Rufiji katika Wilaya ya Ikwiriri,Mkuranga na Kibiti eneo ambalo lilikabiliwa na mauaji ya Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa, Askari Polisi pamoja na watumishi wengine wa Serikali.

Add a comment

Wananchi zaidi ya 40 wakiwemo madiwani kuandamana  zaidi ya kilometa 120 hadi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita june 3 kupinga njama za kutaka kupokonywa ardhi inayozalisha madini ya dhahabu katika machimbo ya Nyakafulu wilayani Mbogwe Mkoani Geita, ambapo tukio hilo limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa kutangaza  kuunda kamati kuchunguza madai hayo. Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 07 Juni, 2019 atakutana na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote hapa nchini na wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC). Wafanyabiashara watano kutoka kila Wilaya hapa nchini watawawakilisha wafanyabiashara wenzao. Mkutano huo utaanza saa 3:30 asubuhi na kurushwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari vya Redio, Televisheni na Youtube Channel ya Ikulumawasiliano. 

 

CHANZO: Ikulu Mawasiliano.

Add a comment

Tanzania imeendelea kuweka juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es Salaam na Mtwara, kujenga bandari kavu na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mbambabay ambayo itawawezesha wafanyabiashara wa Malawi kutumia bandari ya Mtwara.

Add a comment

Wadau wa Uwindaji wa Kitalii wameishukuru serikali ya Marekani baada ya kuondoa zuio kwa kampuni zinazojihusisha na sekta hiyo vya kuuza Nyara za Wanyamapori hasa Simba baada ya kuthibitika kuwa sehemu ya mapato yatokanayo na uwindaji huo yanatumika vyema katika shughuli za Uhifadhi .

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.