Kufuatia migogoro kushamiri kati ya wachimbaji wadogo na uongozi wa kitengo cha ukaguzi na usalama wa mgodi wa Ikuzi wilayani Bukombe ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu, Said Nkumba alitoa siku tatu kuhakikisha Bodi ya ushirika inamuondoa Inspekta mkuu ndugu, Said Manumbu anayelalamikiwa kwa Rushwa ,Bodi ya Ushirika imetengua uongozi wote na kuchangua viongozi wapya kutekeleza Agizo la Mkuu wa Wilaya.
Mwenyekiti wa chama cha Ushirika wachimba madini ya dhahabu Ikuzi Elias Andrea ameongoza Kikao cha Bodi ya Ushirika ili kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya alilowapa kwamba ndani ya siku tatu wawe wameshachagua inspekta mkuu mwingine na kuhakikisha migogoro katika Rashi hiyo inakoma nakufikia mwisho.
Jumla ya mainspekta 20 walioomba nafasi hiyo na baada ya kufanya uchaguzi katibu wa ushirika huo Stanslaus Mkwavi akamtangaza Frank Buhuru kuwa Mkaguzi mkuu atakayeongoza idara hiyo.
Baada ya matokeo hayo mwenyekiti wa ushirika huo Elias Andrea akawaasa waliochaguliwa na kutoa angalizo.
Uchaguzi huo umefanyika chini ya uangalizi wa katibu tarafa ya Siloka ,uongozi wa kijiji cha Ikuzi wa serikali.