Tanzaniani ni miongozi mwa  nchi  12 za Bara la Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotekeleza mradi wa LDFS  lakini bado zinakabiliwa na  uharibifu wa Ardhi ,uwepo wa nusu jangwa, ikolojia iliyobaribika na uzalishaji duni wa chakula kutokana na uharibifu wa mazingara unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa mkaa  na kuharibu vyanzo vya maji.

 

Mratibu wa Mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza uhakika na Usalama wa chakula nchini  LDFS Ngussa Buyamba amesema kuwa  yapo  maeneo yaliobainika kuwa na hali hiyo katika halmsahuri ya Magu, Nzega, Mkalama, Kondoa na Micheweni Tanzania Zanzibar kutokana na uhaba wa Mvua ,ukosefu wa maji na upungufu wa chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Daktari Philemon Sengati akizindua mradi huo unaotekelezwa katika vijiji vya Lumeji,iseni na Nyang'hanga, kata ya Sukuma  wilayani hapa amesema kuwa mradi huo utaongeza tija kwa wakulima ,upatikanaji wa Maji na urejeshaji wa uoto wa Asili uliopote.

 

Utapiamlo na ukosefu wa mavuno ya kutosha ni baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa vijiji hivyo.

  

Utekelezaji wa mradi wa LDFS Ulianza mwaka 2014 nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo Mradi huo unatekelezwa katika nchi 12 za Bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara mbali na Tanzania nchi nyingine  ni Kenya,Malawi,Ephiopia,Uganda,Burundi,Swazland,Nigera ,Ghana,Bukinafaso, Niger na Senegal.

 

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.