Star Tv

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi - Profesa Joyce Ndalichako amezungumza na wasomi wa chuo kikuu cha Iringa-awali kikitambulika kama "chuo kikuu cha Tumaini" Waziri Ndalichako anasema kundi la wasomi kamwe halipaswi kulalamikia changamoto ya ajira, bali linatakiwa kuwa na suruhu kwa kuzalisha ajira katika jamii.

Add a comment

Changamoto ya mimba za utotoni umesababisha zaidi ya wanafunzi 1000 wamekatisha masomo mkoani Mwanza katika kipindi cha miaka mitatu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna amesema kuwa takwimu hizo ni zile zilizotolewa taarifa kwenye madawati ya jinsia ya polisi.

Add a comment

Uongozi wa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara umelazimika kufunga kamera maalumu katika maeneo yote ya hospitali hiyo ili kukabiliana na matatizo ya wizi wa vifaa tiba na vitisho toka kwa ndugu wa wagonjwa kuwapiga wauguzi pindi wanapotoa huduma.

Add a comment

Mfanyabiashara wa vyuma chakavu wilayani Serengeti mkoani Mara imembidi kujisalimisha kwa jeshi la polisi mjini humo baada ya kugundua kauziwa Bomu kwa shilling elfu nne kama chuma chakavu.

Add a comment

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wamewataka wakala wa vipimo WMA mkoa wa Dodoma kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mizani ya wafanyabiashara  ili kuondoa   tabia inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waaminifu ya kuwaibia wateja wao kupitia mizani

Add a comment

Vijana wawili wa Kitanzania, Zakaria Sheha Ally na Shamsi Mwalimu Said wamechukua nafasi ya kwanza na ya tatu kwenye fainali za 27 za tuzo ya kimataifa ya kuhifadhi Quran tukufu. Zakaria Sheha Ally (16) kutoka Tanzania Bara na Shamsi Mwalimu Said (19) kutoka Zanzibar wameibuka na kitita cha dola za Marekani 5,000 na dola 3,000 kila mmoja baada ya kuwashinda wenzao nane waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Afrika Kusini, Sudan, Malaysia, Uturuki, Yemen, Kenya, Burundi na Uingereza.

Add a comment

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Wakurugenzi saba wa Tume ya Umwagiliaji akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Add a comment

Jumuia ya Mabohora Nchini imesema imeanza jitihada za kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli za kuhamia Dodoma kwa kuanza kuhamishia baadhi ya biashara zao mkoni humo.

Add a comment

Ushauri umetolewa kwa wanaume walioko katika wilaya ya Bunda mkoani Mara, kujenga tabia ya kuwasaidia wake zao, ambao ni wajawazito kwa kuwapeleka kliniki na kusikiliza ushauri wa wauguzi, badala ya kuwaacha wenyewe tu kwa kudhani kuwa jukumu hilo ni la mwanamke mwenyewe.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.