Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe ameshauri vyombo vya kutoa haki viweke mikakati ya namna ya

kupunguza mahabusu, akidai kwamba vyombo hivyo kama vitapitia vizuri makosa ya mahabusu hao, itagundua kuwa nusu ya wafungwa walioko

magerezani hawakustahili kuwepo huko. 

 

Mbowe amesema, amekutana na mambo ya kuumiza alipokuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, tangu Novemba 2018 Mbowe

ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam, kuhusu kuondoka kwa Edward Lowassa Mbowe amemtaka kusema ukweli huko aliko na kwamba kukihama chama hicho yalikuwa ni maamuzi yake binafsi. Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni amemwagiza aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuzungumza kile kilichotokea hadi kuvuliwa ubunge. Mbowe amesema halengi kumtetea Nassari lakini amemwagiza kuzungumza na wananchi wa jimbo lake na wanachama juu ya kipi kimetokea. Huku  Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko kwa upande wake amesema hajutii kukaa Segerea kwa sababu amejifunza mengi na ameona mengi,

Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamekaa kwa zaidi ya miezi mitatu gerezani kutokana na kosa la kukiuka masharti ya dhamana.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.