.

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kufuatia majibizano ya risasi baina yao na polisi   wakati wakiwapeleka askari hao ili kuwaonesha katika eneo  la maficho mahala ambapowalikuwa wakitunzia silaha mbalimbali walizokuwa wakizitumia katika matukio kadhaa ya uhalifu  katika eneo la Kiraka Cheusi nje kidogo ya barabara  kuu ya Nyakanazi- Rusumo wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

 

Kamanda wa polisi  mkoa wa Kagera  kamishina msaidizi wa polisi Revocatus  Malimi amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa majibizano hayo yametokea wakati majambazi hao waliokuwa tayari chini ya ulinzi kutakiwa kuonesha maficho ya silaha waliyokuwa wakiitumia inayodaiwa kuhifadhiwa katika   eneo hilo la pori lijulikanalo kama Kiraka Cheusi.

Kamanda Malimi amesema mara baada ya kukamatwa kwa majambazi  katika eneo hilo la Kiraka Cheusi   waliojulikana kwa majina ya Shaban Mangote  mwenye umri wa miaka 40   na Erick Samson mwenye umri wa miaka 19, huku mmoja ambaye hakuweza kutambulika  wote hao walikuwa wanatafutwa kwa kujihusisha na matukio ya utekaji magari na unyang’a nyi wa kutumia silaha katika eneo hilo la kiraka cheusi na ngazi saba wilayani Biharamulo.

Aidha kamanda  Malimi ametoa onyo kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uhalifu kuacha mara moja na kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo endapo watakuwa na mashaka juu ya mtu asiye fahamika.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.