Muamko wa Jamii katika uchangiaji wa damu salama umezidi kukua hali ambayo imesaidia kuokoa maisha ya Wagonjwa wenye uhitaji wa Damu hasa wakinamama wajawaziito na Watoto chini ya umri wa miaka 5 Mkoani Geita, ambapo ukiangalia mwaka 2018  damu iliyokusanywa ni chupa 12,393 sawa na asilimia 62 ukilinganisha mwaka 2017 chupa 5991 sawa na asilimia 34.

Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita awali ilikua ikikabiliwa  na tatizo la damu  kwa upande wa hospital mahitaji ni chupa 150 lakini kwa wastani wa matumizi ni chupa 10 hadi 12 kama hakuna dharura iliyojitokeza. Zaidi ya Wagonjwa 200 kwa siku wanatibiwa  hospitalini hapo.

 

Charles Mateso ,Mratibu huduma ya   Damu Salama Mkoa wa Geita  anasema, baadhi ya watu walikua na mitazamo mibaya kuwa endapo utatoa damu kuna madhara utapata   jambo ambalo si kweli na elimu inayoendelea kutolewa imesaidia wengi kuwa na muamko wa kuchangia damu.

Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri umeendelea kufanya uhamasishaji na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchagia damu kwa hiari.

 
 
 

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.