MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara Charles Kabeho ameongoza zoezi la kuteketeza zao haramu la bangi kavu yenye uzito wa kg 2212 kwa moto iliyo kamatwa na  polisi Tarime Rorya katika kipindi cha miezi saba wakati wa oparesheni tokomeza madawa ya kulevya inayo endelea katika mkoa huo.

Akiongoza zoezi la uteketezaji wa zao haramu la bangi mkuu wa wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amewataka wakulima na wafanya biashara wilayani humo,kuacha kujihusisha na kilimo au biashara ya zao hilo,na badara yake wafanye biashara  halali  zitakazo wasaidia kuwaingiza kipato bila kusumbuliwa na serikali

Kamanda wa polisi mkoa wa polisi Tarime Rorya SACP Henry Mwaibambe amesema mbali na kukamata bangi hiyo pia walifanikiwa kukamata pikipiki 28 na magari 8 yaliyo tumika kusafirisha zao hilo haramu

Jumla ya kesi 15 zenye watuhumiwa 41 wanao jihusisha na biashara ya zao hili haramu la bangi wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Tarime

 

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.