Migogoro ya Adhi katika baadhi ya maeneo hapa nchini imendelea kushamiri licha ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa Amani ambapo wananchi wa wa Kata ya Majengo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamemwomba Waziri wa Ardhi kuingilia kati Mgogoro wa Mipaka unaoendelea baina ya Kata Mbili za  Majengo na Makiba zilizopo kwenye Tarafa ya Mbuguni.

Wakizungumza kwenye Mkutano wa dharura ulioitishwa kwenye Kijiji cha Majengo Kata ya Majengo Wilayani Arumeru,Wananchi hao wakiwemo Viongozi wa Kimiila,Wenyeviti wa Vijiji vyenye Mgogoro pamoja na Viongozi wengine wa Kata, wamesema Mgogoro huo umedumu kwa miaka kumi pasipo kupatikana kwa suluhu ya kudumu.

Baadhi ya wazee kutoka vijiji hivyo Eslesi Manga wa Kijiji cha Engatani pamoja na Saitoti Kooni kutoka Kijiji cha Majengo wamesema Mgogoro huo umekuwa ukiwasababishia vurugu za mara kwa mara na kwamba siku kadhaa zilizopita lilijitokeza tukio la kuchomwa moto kwa  baadhi ya maboma ya wakazi wa Kata ya Majengo.

 Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Majengo Benson Kivondo amesema February 21 mwaka huu maafisa Ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meru walifika eneo hilo kwaajili ya kupima mipaka na kwamba bado matokeo ya vipimo hivyo yameendelea kuibua mkanganyiko na kusababisha sintofahamu kwa Wananchi.

Hata hivyo jitihada za kuutafuta uongozi wa Wilaya ya Arumeru kuzungumzia suala hilo bado zinaendelea. Wilaya ya Arumeru ni miongoni mwa wilaya hapa nchini ambazo kwa kipindi kirefu zimekuwa zikiripotiwa kuwa na migogoro mingi ya ardhi licha ya jitihada kubwa zinazofanya na serikali.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.