Hatimaye Wananchi wa Kijiji cha nyakafuro wakubali kuupokea Mwili wa Marehemu Jackson Charles anayedaiwa kusababishiwa kifo kutokana na kipigo cha polisi  baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga kuingilia kati mgogoro huo na kuwaahidi kufanya uchunguzi wa jambo hilo na kama kuna makosa hatua za kisheria zitachukuliwa.

Machi 24 nido alifariki Marehemu Jackson na Wananchi wakagoma kuzika ambapo mwili ulihifadhiwa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita.

 

Wanakijiji hawa wanaamini kipigo ndio kimesababisha kifo lakini taarifa ya Polisi imeeleza kuwa arehemu alikua na kifafa na Malaria.

Wananchi wanabainisha kuwa ushirikiano wa polisi na Wananchi haupo na kutaka polisi waliokuwepo kubadilishwa.

Wananchi wanaridhia kuzika ambapo Mkuu wa Wilaya ya Geita josephat Maganga ameagiza  uongozi wa Wilaya kutoa ardhi ambapo Serikali ya kijiji imeridhai kwa hilo kwani familia haina eneo na walikua wamepanga tu. 

Siku mbili za uchunguzi zimetolewa na ikibainika  ukiukwaji umefanyika hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kujiridhisha pa kuwa na mashaka.

 

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.