Spika wa bunge la jamuhuri ya Tanzania ndugu, Job Ndugai amewataka watanzania kuonesha uzalendo kwa kutumia ndege za shirika la ndege la Tanzania kuonesha uzalendo na kujivunia kodi yao iliyonunua ndege hizo kwa Mataifa mengine.
Kauli hiyo ameitoa jijini dodoma wakati akihutubia ufunguzi wa ofisi mpya za shirika hilo mjini dodoma. Akizungumza kwenye uzinduzi ndugu Job Ndugai amesema kuwa watanzania wanapaswa kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa shirika lao la ndege kwani raia wa mataifa mengine yenye mashirika ya ndege huthamini ndege za mashirika yao.
Sambamba na hilo amewataka wasimamizi wa shirika hilo kuhakikisha shirika halididimii bali liimarike zaidi. Kwa upande wake waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Isaack Kamwelwe amewatoa shaka watanzania juu ya usalama wa ndege akiwataka kutoogopa kwani kuna usimamizi madhubuti ndani na makapuni yanayotengeza ndege nakutoa pole kwa ajali zilizotokea
Mkurugezi mkuu wa shirika la ndege ATCL amesema kuwa ipo mikakati kadhaa kuhakiksha ndege zinafika maeneo mbalimbali na tayari wameanza safari kwenye maeneo mengine.
Mbali na kufunguliwa tawi hilo shirika la ndege la ATCL limekuwa likifanya safari zake kutoka sehemu mbalimbali na kutua Dodoma kwa muda sasa.