Idara ya uhamiaji mkoani Mara imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 196 toka katika nchi za Afrika ya Kati wakivushwa na kuingizwa nchini kinyume cha sheria na wafanyabiashara wanaofanya biashara za binaadamu waliopo katika mpaka wa Sirali nchini Tanzania na Isibania Nchini Kenya.

Mkuu wa idara ya uhamiaji mkoa wa Mara naibu kamishina wa uhamiaji Fredrick Kiondo ametoa taarifa hizo katika semina ya kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa idara mbali mbali za serikali toka katika nchi za Kenya na Tanzania ili waweze kukabiliana na tatizo la wakimbizi na wahamiaji haramu.

Nae mkuu wa wilaya ya Kuria kasikazini toka nchini Kenya Gatungu Machira ameelezea juu ya wakimbizi na wahamiaji haramu wapitao katika wilaya yake anasema kuwa ni muhimu kwa serikali hizi mbili kushirikiana kukabiliana na tatizo hilo.

Akifungua warsha hiyo mkuu wa wilaya ya Tarime mhandisi Charles Kabeho amewataka viongozi kuondokana na tatizo la kuwaficha watu wanaofanya biashara ya bianadamu katika mpaka wa Sirali.

Hivi karibuni wakimbizi zaidi ya 56 wakiwemo wadogo 30 walikamatwa wilayani Tarime wakiwa katika basi wakitokea katika kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo mkoani Kigoma wakielekea nchini Kenya huku wakitajwa kuvuka vizuizi vingi ndani ya nchi.

 

Idara ya uhamiaji mkoani Mara imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 196 toka katika nchi za Afrika ya Kati wakivushwa na kuingizwa nchini kinyume cha sheria na wafanyabiashara wanaofanya ya biashara za binaadamu waliopo katika mpaka wa Sirali nchini Tanzania na Isibania Nchini Kenya.

 

 

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.