Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wamewataka wakala wa vipimo WMA mkoa wa Dodoma kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mizani ya wafanyabiashara ili kuondoa tabia inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waaminifu ya kuwaibia wateja wao kupitia mizani
Wizi huo hufanywa kwa kuwekewa mawe katika moja ya vyuma vya mizani na kusababisha mnunuzi kupata kilo hafifu tofauti na thamani ya fedha alizo toa
baadhi ya wanunuzi wanaofika kupata mahitaji katika maduka na magulio wamesema pamoja na kuwepo na kuanza kwa maazimisho ya wiki ya vipimo duniani zoezi hili lifanywe mara kwa mara ili kudhibiti kitendo hicho kwa wafanyabiashara wasio waaminifu. Kaimu meneja wakala wa vipimo mkoa wa Dodomaa Joachim Dotto amesema lengo la ukaguzi huo ni kumlinda mlaji ambapo litakuwa endelevu kwa kushirikiana na Jeshi la polisi.
.