Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amewahimiza Waislamu hasa wanaokaa katika mikoa yenye dhahabu kuondoka katika hali ya kawaida ya kuendeisha dini tupu bali iwe dini na uchumi kwa lengo la kuwa tegemezi lakini kuwa na uchumi imara utatoa fursa ya kujisimamia na kuendesha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Ni ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi amefanya ziara ya siku mbili lengo ni kutembelea na kuona miradi na uwekezaji uliofanya na viongozi wa kiislam katika mkoa wa Geita, na kubainisha kuwa zama za sasa ni za kuleta maendeleo na sio migogoro ambayo inadidimiza juhudi za kuleta maendeleo. Baraza kuu la Waislamu Tanzania makao makuu limeanzisha kitengo cha uchumi na maendeleona huku viongozi wakitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha fursa zilizopo mlangoni zinatumika huku Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akisema kuwa Viongozi wana wajibu wa kuibadilisha jamii hasa kwa kuwaongoza kwa maadili ambayo yanampendeza Mungu yenye kutoa haki pasi na ubaguzi. Mufti Zubeir amezindua msikiti Buseresere Wilayani Chato, Kiwanja cha ujenzi shule ,eneo la uchimbaji wa dhahabu Wilayani Bukombe na Mradi wa Shule Geita Mjini.