Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Wakurugenzi saba wa Tume ya Umwagiliaji akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

 “CAG afanye haraka uchunguzi wa kina, tunataka kujua ni nani alikuwa mlango wa ubadhirifu huu. Hatutamuonea mtu, wote watakaothibitika kuhusika na matumizi mabaya ya fedha watachukuliwa hatua.” Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo  wakati wa kikao na viongozi wa tume hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu. Mbali na kuwasimamisha kazi wakurugenzi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi wengine 21 wa tume hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na utendaji usioridhisha kwenye miradi mbalimbali inayosimamiwa na tume hiyo. Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua hiyo kutokana na udhaifu wa kiutendaji ndani ya tume hiyo ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za miradi, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo na kukosa umakini. “Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya ubadhirifu uliofanyika katika miradi ya umwagiliaji.” Amesema hali ya kilimo cha umwagiliaji nchini hairidhishi na Serikali haijafurahishwa na utendaji wa Tume ya Umwagiliaji licha ya kuwekeza nguvu kubwa, hivyo inataka kuona mabadiliko.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amesema miradi mingi ya umwagiliaji ilifeli kwa sababu ya ilijengwa chini ya kiwango hususani mabwawa na pia haikuwa ikilingana na kiasi cha fedha kilichokuwa kinatolewa. “Mradi wa kutumia sh. bilioni mbili wanatumia sh. bilioni nne.”

 

CHANZO: Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.