Star Tv

Waziri Lukuvi aingilia kati Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 baina ya wanakijiji wa mkwajuni kata ya vijibweni wilaya ya kigamboni jijini Dar es salaam na mwekezaji kutoka Korea na kuagiza kupitiwa upya kwa mchakato uliosababisha mgogoro huo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata haki zao.

Ni katika ziara ya siku moja ya Waziri wa Ardhi nyumba na maendleo ya makazi William Lukuvi katika kata ya vijibweni kigamboni jijini Dar es salaam kwalengo la kusikiljza malalamiko ya wananchi juu ya mgogoro wa Ardhi baina  yao na mwekezaji kutoka nchini  Korea ambaye anataka kutumia eneo hilo kujenga Chuo Kikuu.

Aidha, Waziri Lukuvi amepiga marufuku wenyeviti wa Serikali za mitaa na vijiji kutumia mihuli yao kuidhinisha ununuaji wa viwanja. Baadhi ya wakazi wa Kata ya Vijibweni Kigamboni Jijini Dar es salaam wametumia ziara hiyo ya Waziri Lukuvi kupaza sauti zao juu ya kukithiri kwa migogoro ya ardhi wilayani humo.

Ziara hiyo ya Waziri Lukuvi Manispaa ya Kigamboni ni mwendelezo wa Waziri huyo kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuhimiza na kusimamia matumizi sahihi ya ardhi na kutafuta suluhisho la migogoro ya ardhi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.