Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi - Profesa Joyce Ndalichako amezungumza na wasomi wa chuo kikuu cha Iringa-awali kikitambulika kama "chuo kikuu cha Tumaini" Waziri Ndalichako anasema kundi la wasomi kamwe halipaswi kulalamikia changamoto ya ajira, bali linatakiwa kuwa na suruhu kwa kuzalisha ajira katika jamii.
Vijana wametakiwa kuachana na fikra za kutaka kuajiriwa, bali wawe wazalishaji wa ajira katika jamii, ili kwenda sambamba na mbio za serikali ya awamu ya tano inayokimbizana kutaka uchumi wa viwanda, unaotajwa kumaliza tatizo la ajira. Mkurugenzi wa kitengo cha ujasiriamali na ubunifu katika chuo kikuu cha Iringa- Deo Sabokwigina, anasema kuanzishwa kwa masomo ya ujasiriamali kwa vitendo katika chuo kikuu cha Iringa kumesaidia kuongeza soko la ajira.